Polisi Yamkabidhi Manji Mahakamani Baada ya Kumaliza Kumuhoji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi Yamkabidhi Manji Mahakamani Baada ya Kumaliza  Kumuhoji
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkabidhi mfanyabiashara Yusuf  Manji na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza kumuhoji katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa kama Mahakama ilivyoamuru warudishwe baada ya Polisi kumaliza kuwahoji.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama ilivyo awali, ambapo ameahirisha hadi September 8, 2017.

Awali Mahakama hiyo iliruhusu Yusuf Manji na wenzake watatu kwenda kuhojiwa na Polisi kwa lengo la kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi wanayokabiliwa nayo.

Mbali na Yusuf Manji, washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza Stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.






----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad