Taarifa Kuhusu Ali Kiba Kuiba Wimbo wa Seduce..Mwenyewe Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamuziki Ali Salehe Kiba amepangua tuhuma za kuiba wimbo unaosumbua kwa sasa mtaani 'Seduce Me ' na kusema kuwa katu kitu kama hicho hakitaweza kikatokea kwenye maisha yake na kuwatoa hofu mashabiki zake wasiumizwe na maneno kwani anajiamini.

Alikiba amelazimika kupangua tuhuma hizo baada ya kuwepo na maneno mitandaoni ya kwamba wimbo wa 'Seduce Me' uliotengenezewa na mtayarishaji Man Water umfanyiwa  'copy' kutoka kwenye wimbo ulioimbwa na kwa lafudhi ya kiharabu .

"Siyo kweli kama nimeiba wimbo. Hicho ni kitu ambacho sijawahi kufanya na hakitaweza kutokea kwenye maisha yangu yote kwa sababu najiamini. Nawaomba mashabiki zangu waendelee kufurahia muziki mzuri. Duniani kote nyimbo ambazo zimefanya vizuri zimetengenezewa 'cover' nyingi sana, hivyo ndivyo ilivyotokea kwenye wimbo wangu kwahiyo nawasihi mashabiki zangu wasiogope kwa kudhani nimeiba wimbo wa mtu" alisema Alikiba.

Pamoja na hayo Alikiba amewasihi mashabiki zake wasiwe na hofu kwani hawezi kukaa kimya kwa muda mrefu kwani mwaka huu amepanga kuwafurahisha na pindi watakapokuwa wanataka ngoma mpya wasisite kumtaarifu ili aachie kazi nyingine mpya.

Kwa sasa Alikiba anasumbua na ngoma inayokwenda kwa jina la 'Seduce Me' iliyotoka Agosti 25 ambapo mpaka sasa inawatazamaji zaidi ya milioni 4 katika mtandao wa YouTube kupitia account yake ya 'Vevo'.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad