TANZIA: Don William Afariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TANZIA: Don William Afariki Dunia
MKALI wa muziki wa country, Donald Ray Williams ‘Don Williams’, amefariki dunia. Williams alifariki jana Ijumaa akiwa nyumbani kwake Alabama, nchini Marekani.
Williams aliyekuwa maarufu duniani kote kwa muziki wa country, alitamba na vibao kadhaa kikiwamo kile cha ‘I Believe in you’ alichokitoa mwaka 1981, amefariki dunia akiwa na miaka 78 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mbali na ‘I Believe in you’, vibao vingine maarufu vya Williams ni pamoja na Some Broken hearts never mend, Love me tonight, Lay down beside me na vinginevyo.
Pamoja na umaarufu wake katika muziki, Williams hakuwa mtu mwenye makuu na aliyapenda maisha ya kawaida kiasi cha kubatizwa jina la “the Gentle Giant”.

Williams aliyezaliwa mwaka 1939, alianza kupenda muziki akiwa Portland kabla ya kuhamia Nashville miaka ya 1960 ambako umaarufu wake ulitapakaa duniani kote.
 
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad