Tuliowakamata Jana kwa Kufanya Mkusanyiko Usio Rasmi Lazima Tuwashughulikie- Mambosasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tuliowakamata Jana kwa Kufanya Mkusanyiko Usio Rasmi Lazima Tuwashughulikie- Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema watu waliokamatwa na polisi hapo jana kwa kufanya mkusanyiko usio rasmi, walishaonywa kutofanya hivyo lakini hawakujali hivyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yao.

Kamanda Mambosasa amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, na kusema  kitendo cha kufanya mkusanyiko usio rasmi ni kuvunja sheria, hivyo lazima watafikishwa Mahakamani kujibu shtaka lao, huku akikanusha kuwakamata watu hao kwa kutokana na kuvaa  t-shirt zilizoandikwa 'pray for Tundu Lissu'.

"Kwanza ifahamike hatujawakamata kwa kosa la kuvaa tshirt, zile ni nguo kama nguo nyingine wanavyovaa mashabiki wa Simba na Yanga, hawa walichofanya mpaka wakamatwe ni kufanya mkusanyiko usio rasmi na kibaya zaidi tulishawaeleza, na wenyewe walipoona polisi wanakuja wakaanza kutukimbia kwamba walijua wamefanya nini", amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa ameendelea kwa kusema  jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watu hao na kisha kupelekwa Mahakamani kusomewa mashtaka yao ili sheria ifanye kazi yake.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad