Wanne Wauawa na Washukiwa wa al-Shabab Lamu, Kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu Wanne Wauawa na ashukiwa wa al-Shabab Lamu, Kenya
Watu wanne wameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab katika eneo la Hindi katika kaunti ya Lamu katika eneo la pwani nchini Kenya.
Kamishna wa kaunti hiyo Gilbert Kitiyo ameambia BBC kwamba maafisa wakuu wa usalama katika kaunti hiyo wanakutana na watatoa maelezo zaidi baada ya mkutano huo.

Gazeti la kibinafsi la Standard linasema wakazi wamejitokeza barabarani katika mji huo kuandama kulalamikia 'kukawia' kwa maafisa wa usalama kufika eneo la shambulio.
Kenya yaanza kuangusha mabomu ‘msitu wa al-Shabab’

Kisa hicho kimetokea siku chache baada ya watu watatu kuuawa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la al-Shabab waliposhambulia basin a gari eneo la Nyongoro, Witu katika kaunti hiyo ya Lamu.

Gazeti la Standard linasema visa vya mashambulio vimeongezeka eneo hilo wiki za hivi karibuni.
Kamishna wa kanda ya Pwani Nelson Marwa majuzi alitangaza kwamba maafisa wa usalama wangeanza kuangusha mabomu katika msitu wa Boni ambapo wanamgambo wa kundi hilo la Kiislamu wanadaiwa kujificha.
Wakazi waliokuwa wakiishi msituni na karibu na msitu huo walitakiwa kuhama
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad