Auwawa kwa Kupigwa Risasi na Wahalifu Wenzake Akiwa Chini ya Ulinzi wa Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Auwawa kwa Kupigwa Risasi na Wahalifu Wenzake Akiwa Chini ya Ulinzi wa Polisi
Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Robert Massawe (51), ambaye polisi wanadai ni mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake.

Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo mbalimbali na laini za simu 58.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo.

Amesema mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki.

Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam.

Kamanda Issah amesema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufanya tukio la ujambazi katika Kijiji cha Chilio, Kata ya Holili wilayani Rombo jana alfajiri.

Amesema askari walifuatana naye chini ya ulinzi hadi Moshi kwenye dampo lililopo jirani na kiwanda cha ngozi ambako bunduki ilifukiwa ardhini ikiwa na risasi 24.

“Chini ya ulinzi wa askari kanzu, alipowaona wenzake alipiga kelele kuwajulisha polisi walikuwepo eneo hilo,” amesema.

Kamanda Issah amesema kelele ziliwafanya watuhumiwa hao kukimbia huku wakifyatua risasi hovyo na baadhi zilimpiga Massawe mkono wa kushoto, mgongoni na mguuni hivyo kusababisha kifo chake.

Polisi imesema mtuhumiwa alishiriki matukio manane ya uporaji wa fedha na mauaji kwa kutumia silaha na amewahi kufungwa kwa ujambazi lakini aliachiwa baada ya kukata rufaa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad