Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Kenya Roselyn Akombe IEBC Ajiuzulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Kenya Roselyn Akombe IEBC Ajiuzulu
Mmoja wa maafisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Dkt. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika tume hiyo chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi mpya wa urais kufanyika nchini humo.
Ametangaza kwamba anahofia usalama wake na hatarajii kurejea Kenya hivi karibuni.
Dkt Akombe ametuma taarifa kutoka mjini New York anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.
Katika taarifa, Dkt Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.

Tume ya IEBC imesema imesikitishwa na hatua ya Dkt Akombe kujiuzulu na kuahidi kutoa taarifa ya kina baadaye. Mwenyekiti Wafula Chebukati anatarajiwa kuhutubia wanahabari baadaye leo.

"Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC utawasikitisha baadhi yenu, lakini si kwa sababu nilikosa kujaribu. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu ukizingatia hali na mazingira yaliyopo. Wakati mwingine, unalazimika kusalimu amri na kuondoka, hasa wakati maisha ya watu yamo hatarini," amesema kwenye taarifa hiyo.
"Tume sasa imekuwa kama sehemu ya mzozo wa sasa. Tume imo matatani."

"Imekuwa vigumu kuendelea na mikutano ya tume ambapo Makamishna kila wakati wanalazimika kupiga kura kufanya maamuzi kwa kufuata msimamo wao badala ya kuangazia uzito wa jambo linalojadiliwa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad