Serikali Kununua Meli Itakayofanya Kazi Bukoba na Mwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali Kununua Meli  Itakayofanya Kazi Bukoba na Mwanza
Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania imetangaza tenda ya kununua Meli itakayokuwa inafanya safari zake kwenye ziwa Victoria kati ya Miji ya Bukoba na Mwanza.

Hilo limebainishwa leo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam, wakati akitoa hotuba baada ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa kamati ya Madini iliyofanikisha uchunguzi wa Mchanga wa madini (Makinikia) pamoja na mikataba ya madini kati ya serikali na kampuni ya Barrick.
“Fedha zipo nyingi ndio maana tunaweza kuanzisha miradi mbalimbali na sasa tumetangaza tenda ya kununua na kujenga Meli mpya itakayokuwa inafanya kazi ziwa Victoria kwasababu hakuna Meli tangu ndugu zetu wapoteze uhai kwenye ajali ya MV Bukoba”, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais ameongeza kuwa tayari nchi ya Korea ya Kusini imeshaonesha nia ya kuchukua Tenda hiyo ya kununua na kujenga Meli itakayokuwa inatoa huduma ndani ya ziwa Victoria.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. "Mtoto acha kupiga mayowe, acha waje waone wenyewe", kazi kazi tu, hapa reli, kule ndege, huku meli kinaeleweka.

    ReplyDelete

Top Post Ad