Weah Kuchuana Tena na Boakai Novemba 7 Katika Uchaguzi wa Marudio

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Weah Kuchuana Tena na Boakai Novemba 7 Katika Uchaguzi wa Marudio
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Alhamisi iliweka rekodi ya kutangaza rasmi matokeo yote ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 10 ikiwa ni siku sita kabla ya tarehe ya mwisho iliyopangwa Oktoba 25.

Ikitangaza matokeo hayo, NEC imethibitisha kwamba mwanasoka nyota wa zamani duniani, George Weah aliyewania urais kupitia chama cha Congress For Democratic Change (CDC) atachuana na Makamu wa rais Joseph Boakai wa chama tawala cha Unity Party (UP)

Katika uchaguzi huo wa marudio uliopangwa Novemba 7, mshindi ataapishwa kuchukua nafasi ya Rais Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake.

Sirleaf alishinda kwa mara ya kwanza urais mwaka 2006 kuwa rais wa kwanza barani Afrika kuchaguliwa kidemokrasia. Alishinda muhula wa pili mwaka 2011 na atakabidhi madaraka kwa rais wa pili tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomalizika mwaka 2003.

Baada ya kujumlisha matokeo yote kutoka vituo 5390 vya kupigia kura vilivyosambaa nchi nzima hakuna mgombea aliyepata asilimia 50+ ya kura za kumwezesha kuwa rais.

Weah alipata kura 596,037 sawa na asilimia 38.4, Boakai kura 446,716 sawa na asilimia 28.8, Cahles Brumskine wa LP kura 149,495 (9.6%), Prince Johnson wa MDR kura 127,666 (8.2%), Alexander Cummings wa ANC kura 112,067 (7.2%) na Benoni Urey wa ALP kura 24,246 (1.6%)

Wagombea wengine 14 waliambulia chini ya asilimia moja ya kura. Wapigakura 1,641,922 sawa na asilimia 75.2 ya waliojiandikisha walishiriki uchaguzi huo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad