Zitto Kukimbilia Mahakamani Kupinga Uteuzi wa Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kukimbilia Mahakamani Kupinga Uteuzi wa Rais Magufuli
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) amesema Jumatano hii ataenda Mahakamani kupinga uteuzi wa nafasi ya Katibu wa Bunge uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli Jumamosi iliyopita.


Uteuzi huo ulienda sambamba na uteuzi wa Mawaziri ambapo baadhi ya mawaziri walibadilishwa na wengine kuongezwa.

“Katika kulinda utawala wa sheria nchini kwetu, pia Uhuru na Hadhi ya Mhimili wa Bunge, Leo tarehe 11/10/2017 tunawasilisha mahakamani ombi la kutengua uteuzi wa Katibu wa Bunge na kutaka mchakato wa kisheria ufuatwe katika kumpata Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” aliandika Zitto Facebook.

Rais Magufuli alimteua Katibu mpya wa Bunge na yule ambaye alikuwa akifanya shughuli hiyo kuahidi kumpangiwa kazi nyingine.

Zitto alisema uteuzi wa Katibu wa Bunge uliofanywa na Rais John Magufuli ni batili Kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge, sheria namba 14 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na Katiba ya JMT ibara ya 87.

Alisema Katiba inatoa Mamlaka Kwa Rais kuteua na sheria inaweka utaratibu Wa kutekeleza mamlaka hayo ya Katiba.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Angry Face... Umerudi tena Mtandaoni?
    Mbona Magu ameshateua ... Jina lako sikuliona?
    Au Ndiyo yale yale... !!! na Wewe Ndiyo Yule yule.
    Pole Dogo.... Mie naona Uduvi umekuwa Dagaa...!!!
    Au.... Dagaa wamekuwa Uduvi?
    Dogo tafuta ustaarabu mwingine... Ya NSSF Kigamboni yako njiani... Huwezi Kutulia chectu.

    ReplyDelete
  2. Angry Face... Umerudi tena Mtandaoni?
    Mbona Magu ameshateua ... Jina lako sikuliona?
    Au Ndiyo yale yale... !!! na Wewe Ndiyo Yule yule.
    Pole Dogo.... Mie naona Uduvi umekuwa Dagaa...!!!
    Au.... Dagaa wamekuwa Uduvi?
    Dogo tafuta ustaarabu mwingine... Ya NSSF Kigamboni yako njiani... Huwezi Kutulia chectu.

    ReplyDelete

Top Post Ad