Frank Lampard Amkingia Kifua Mourinho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Frank Lampard Amkingia Kifua Mourinho
Nyota wa zamani na mfungaji wa muda wote wa klabu ya Chelsea Frank Lampard, amemkingia kifua kocha wa Manchester United kuwa hastahili lawama endapo hatotwaa ubingwa wa England msimu huu.
Lampard ambaye alitwaa mataji matatu ya EPL chini ya Mourinho amesema ikitokea kocha huyo hajatwaa ubingwa wa EPL msimu huu hastahili lawama bali lawama ziende kwenye ubora wa wachezaji alionao kwenye timu.
“Mourinho ni kocha anayependa kushinda na hufundisha mbinu ya kushinda tu tofauti sana na makocha wengine kama Pep Guardiola ambaye hufundisha pia kucheza mpira wa kuvutia hivyo inapokuja suala la kutopata matokeo ni ubora wa wachezaji na sio Mourinho”, amesema Lampard.
Siku za hivi karibuni Mourinho amekuwa akikosolewa kuhusu mfumo wake wa uchezaji wa kujilinda zaidi ambao awali haukuwa unatumiwa na Manchester United, ambayo ilizoeleka kwa kushambulia zaidi kuliko kujilinda.
Manchester United ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 23 nyuma ya vinara, mahasimu wao wa jiji Manchester City ambao wana alama 31 katika michezo 11 ya msimu huu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad