Irene Uwoya Atua na Mwanaye Kigali Kuhani Msiba wa Aliyekuwa Mume Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Irene Uwoya Atua na Mwanaye Kigali Kuhani Msiba wa Aliyekuwa Mume Wake
Mrembo wa zamani wa taji la Miss Chang’ombe na mwigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amewasili jijini Kigali, Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewe, Ndikumana Hamad.

Ndikumana aliyekuwa akijulikana kama Katatut, alifariki dunia ghafla siku chache zilizopita na kuzikwa juzi jijini Kigali.

Uwoya hakuwa jijini Kigali wakati wa mazishi na usiku wa kuamkia leo ametua jijini Kigali akiongozana na mwanaye, Klishy ambaye alizaa na marehemu. Pia aliongozana na mama yake mzazi.

Uwoya alijifunika sura muda wote wakati akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kanombe jijini Kigali.

Wakati anatua, ndugu wakiwemo mashabiki wa michezo na burudani, walijitokeza uwanjani hapo.

Kataut ambaye alicheza soka katika nchi kadhaa za Ulaya, mauti yalimkuta akiwa kocha msaidizi wa Rayon Sports na siku moja kabla ya kifo chake alikuwa mazoezini.

Kwa hapa nchini, Kataut aliwahi kuichezea Stand United kabla ya Kocha Patrick Liewig raia wa Ufaransa, kupendekeza aachwe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad