Katambi Awajia Juu Chadema "Nimekaa Kimya Kuficha Haiba Yao Wasiponiomba Radhi Nitasema Kilichonitoa Kule"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katambi Awajia Juu Chadema "Nimekaa Kimya Kuficha Haiba Yao Wasiponiomba Radhi Nitasema Kilichonitoa Kule"
Aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amewataka viongozi wakuu wa Chadema kuthibitisha tuhuma za kununuliwa kwake na CCM la sivyo atatoa sababu za kina za uamuzi wa kuhama chama hicho.

Katambi Jumanne Novemba 21,2017 alitangaza kujiunga CCM katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam akidai upinzani hauna dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi.

Akizungumza na Mwananchi  leo Alhamisi Novemba 23,2017, Katambi amesema, “Inaniuma kuona nazushiwa uongo, natishwa kwa uamuzi wangu, nilikaa kimya kulinda staha za watu, nimetoa muda  wathibitishe wanachokisema.”

Amesema, “Unajua hekima na busara zangu zilinilazimisha kuondoka Chadema na kuhamia CCM bila kufafanua yaliyonitoa ili kuacha haiba yao waendelee kwa amani na mfumo wao wa siasa mpya, lakini wameshindwa sasa nitasema ukweli kama watashindwa kudhibitisha hadharani.” Katambi amesema hakukurupuka kufikia uamuzi wa kuondoka Chadema na wala hakuwashirikisha wazazi wake, kwa hiyo anayepaswa kulaumiwa au kutishwa ni yeye si wazazi au mke wake.

“Nimekuwa nikipokea vitisho vya kila aina, wazazi wangu na mke wangu, niseme tu kwamba mlinzi wa kwanza wa maisha yangu ni Mungu. Namwachia Mungu maisha yangu niliyoyatoa katika ukweli kwa faida ya Watanzania,” amesema.

Amesema kama watashindwa kutoka hadharani kukanusha taarifa hizo, ataitisha mkutano na waandishi wa habari na kusema ukweli wa kile kilichomfanya akaondoka Chadema.

Jana Jumatano Novemba 22,2017 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na Mwananchi alisema Katambi hakuondoka hivihivi bali kuna hila ilifanyika ambayo ilitumia saa 48 kukamilisha mchakato na kujiondoa.

"Badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashawishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa."
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha kututishia wew sema akuna anae kuogopa uwezi kuiangusha chadema wewe na mtu mdogo saaana huwezi shindana na nguvu ya uma

    ReplyDelete
  2. Muogopeni Mungu vijana.

    ReplyDelete
  3. shiiida yote njaaa hiyo inawapelekesha unatisha kama ulivyotishwa sio chadema ndio mpango mzima wewe ile nguvu ya umma sio familia unaogopa njaa mjomba uzalendo umekushinda

    ReplyDelete
  4. Acha uongo. Hata uso wako unaonekana unadanganya. Useless people.ulipewa nguvu na kulelewa leo unatoa pumba za uongo. Huna hata aibu

    ReplyDelete
  5. Kitambi... Karibu sana Nyumbani.
    Hawa wanao Haaa haaaa wanajua mchango wako na pigo walilo lipata.
    Vijana kama wewe ilikuwa nguzo kwa mfumo wao wa upingaji wa kila kitu.
    na uliwasaidia kiasi kikubwa kwa kampeni wa kile walicho kiita UKUTA katika uhamasishaji.
    Leo wanakuona ni Adui mpaka wakuvishe TUHUMA za KUNUNULIWA na CCM.
    Mbowe na tuma zake tutazishughulikia.

    ReplyDelete

Top Post Ad