Kocha Afunguka Kuhusu Atakayeziba Nafasi ya Mbwana Samatta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kocha Afunguka Kuhusu Atakayeziba Nafasi ya Mbwana Samatta
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga ameweka wazi kuwa nafasi ya nahodha wa kikosi hicho Mbwana Samatta itazibwa na wachezaji ambao amewaita ndani ya kikosi hicho.
Samatta ambaye anakipiga kwenye ligi ya Ubeligji katika klabu ya KRC Genk ameumia misuli ya paja hivyo kulazimika kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita kwaajili ya matibabu.Hiyo inamaanisha Samatta ataukosa mchezo wa Novemba 12 dhidi ya Benin.
Kocha Mayanga amekiri kuwa ni pengo kumkosa nahodha huyo lakini kama timu hawana budi kukubali na kutafuta namna ya kuziba nafasi yake kupitia wachezaji 24 ambao amewaita kwenye kikosi hicho.
“Ni kweli tumepata pengo kumkosa Samatta ambaye ni nahodha lakini hatuna namna lazima tukubaliane na hali halisi, lakini tunaowachezaji wanaoweza kuziba nafasi hiyo wakiwemo vijana tuliowaita kutoka timu za vijana”, amesema Mayanga.
Taifa Stars itasafiri kuelekea Benin ambako itacheza mchezo wa kalenda ya shirikisho la soka la kimataifa FIFA, Novemba 12.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad