Magufuli na Museveni Waweka Historia kwa Kuweka Jiwe la Msingi Bomba la Mafuta Uganda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Magufuli na Museveni Waweka Historia kwa Kuweka Jiwe la Msingi la Bomba la Mafuta Uganda
MARAIS John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda waliweka historia jana baada ya kuzindua kituo cha pamoja cha forodha kitakachochochea ukuaji wa biashara kwa nchi zote mbili.

Kituo hicho cha aina yake, kipo katika mpaka wa Tanzania na Uganda, eneo la Mtukula.

Magufuli (maarufu JPM), ambaye yuko nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, alisema wakati wa ufunguzi wa kituo hicho na mwenyeji wake, Museveni,  kuwa wafanyabiashara waliokuwa wakitumia muda mrefu kutoa mizigo katika eneo hilo sasa wataondokana na adha hiyo.

Alisema kumekuwa na ukwamishaji wa maendeleo baina ya viongozi na wafanyabiashara wanaopeleka na kuingiza bidhaa ndani ya nchi hizo kwa kufanya ukaguzi wa muda mrefu  unaomfanya mtu kutumia zaidi ya dakika 20.

Rais Magufuli alisema  kituo cha Mtukula  kilikuwapo tangu mwaka 2011 na kuanza kufanya kazi mwaka 2015, huku kikitoa huduma kwa muda mrefu ili kukamilisha utaratibu.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, kituo hicho kimegharimu Sh. bilioni 7.16 hadi kukamilika kupitia fedha iliyotolewa na Trademark East Afrika kupitia ufadhili wa Canada na Uingereza.

Naye Rais Museveni alisema katika  kupanua sekta ya uchumi na maendeleo, shughuli za kilimo, ufugaji, viwanda ni nguzo katika kutoa ajira kwa wananchi wa Uganda na Tanzania.

Katika ziara hiyo ambayo Rais Magufuli ameongozana na mke wake, Mama Janeth Magufuli, yeye pamoja na Museveni walifungua walifungua  kituo cha pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) kilichojengwa kwa lengo la kurahisisha taratibu za kiforodha, uhamiaji na kuharakisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Sambamba na kufungua kituo hicho, marais hao jana waliweka jiwe la msingi katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la kuanzia Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Sherehe hizo zilifanyika katika kijiji cha Luzinga, kilichoko katika mkoa wa Rakai nchini Uganda.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad