Mchezaji Yanga Amfata Kocha Lwandamina Kumpa Ruhusa ya Kuondoka Kwenye Klabu Hiyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mchezaji Yanga Amfata Kocha Lwandamina Kumpa Ruhusa ya Kuondoka Kwenye Klabu Hiyo
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Matheo Anthony, hivi karibuni aliamua kumfuata kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, akitaka kumpa ruhusa ya kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuchoka kukaa benchi.
Matheo aliyejiunga na Yanga akitokea KMKM ya Zanzibar, mara kwa mara amejikuta akikosa nafasi ya kutumika kwenye kikosi cha kwanza ambapo kwa sasa straika huyo amejiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kwa ajili ya michuano ya Chalenji ambayo itaanza kutimua vumbi Desemba 3, nchini Kenya.
Chanzo kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatatu kuwa, mshambuliaji huyo alikuwa na kikao na Lwandamina akitaka amruhusu kuihama timu hiyo kwa sababu ya kukosa namba ambapo Kagera Sugar wamekuwa wakimtaka.
“Kweli kabisa hivi majuzi kocha Lwandamina aliongea na Matheo, kwa ajili ya kutaka aruhusiwe kwani amechoka suala la kukaa benchi.
“Na huenda kwenye dirisha hili la usajili anaweza kuondoka kwani Kagera Sugar wamekuwa wakimtaka kwa ajili ya kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi chao,” kilisema chanzo hicho.
Championi Jumamosi, lilimtafuta Matheo ambapo alisema: “Kweli nimeongea na kocha, Lwandamina kumuomba aniruhusu niondoke kwani nimechoka kukaa benchi.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad