Suluhu ya Lipuli Yawatesa Simba Haji Manara Amtupia Lawama Muamuzi wa Mchezo Huo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Suluhu ya Lipuli Yawatesa Simba Haji Manara Amtupia Lawama Muamuzi wa Mchezo Huo
Msemaji Mkuu wa klabu ya Simba SC, Haji Manara ameendelea kuwalalamikia waamuzi wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa kushindwa kuchezesha vizuri mechi zote za timu yake.

Manara amesema hayo mapema baada ya timu yake kulazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya klabu ya Lipuli FC kutoka mkoani Iringa.

“Naomba kwenye suala la uamuzi bodi ya ligi kama vile inavyochukuaga uamuzi kwa wachezaji, wakati mwingine wanawapa adhabu kali kuna mchezaji alifungiwa miaka miwili wakati mwingine wasemaji wanafungiwa mwaka mmoja, bodi ya ligi na TFF kama mnaridhika kabisa mwamuzi huyu amechezesha sivyo kwa makosa yaleyale na rekodi zilezile, chukueni hatua kubwa isiishie tu kumsimamisha.”amesema Haji Manara mapema baada ya mchezo kumalizika huku akimlaumu Mwamuzi wa mchezo wa leo dhidi ya Lipuli FC.

“Maana adhabu kubwa utasikia amesimamishwa hata malizia mzunguko huu, pigeni kifungo au kufuta waamuzi wa hovyo, hakuna kitu kinachoumiza mpira wa Tanzania kama uamuzi mbovu. Nasema matokeo yake naonekana kama mkorofi, mlalamishi au nawaonea waamuzi lakini macho yote yanaona na mmeshuhudia pale kilichotokea, tumenyimwa penati ya wazi lakini sitaki kulalamika, nikilalamika ntaonekana nalalamikia waamuzi, chukueni hatua kama mkiridhika waamuzi hawachezeshi vizuri.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad