Waziri wa Afya Apiga Marufuku Uuzwaji wa Damu Katika Vituo vya Afya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Afya Apiga Marufuku Uuzwaji wa Damu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameendelea kusisitiza kuwa wananchi hawapaswi kununua damu kwani huduma hiyo ni bure kwa watanzania wote katika hospitali zote.

Hayo amezungumza leo jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait katika Taasisi ya Mifupa MOI ambapo uliuzuliwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania.

“Watanzania wanahoitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure marufuku kwa watoa huduma za vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani inatoka kwa wananchi wenyewe” alisisitiza Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza katika kuchangia damu ili kuweza kuwa na hifadhi ya kutosha na kufanya kazi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kwa wakati sahihi bila ya usumbufu wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa anayo furaha kutimiza miaka miwili tangu kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kupiga hatua katika sekta ya afya hasa katika kupunguza rufaa za nje na kuwa na utaalamu wa matibabu ya kibingwa kama vile upandikizaji wa figo, vifaa vya usikivu( Coclea Impant) na kutibu magonjwa ya moyo.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem amesema kuwa wameamua kuchangia kiasi cha fedha cha shilingi Milioni 200 katika kutengeneza Benki hiyo ya damu MOI ili kuweza kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini.

“Mbali na kiasi hicho cha fedha pia tumetoa Dola za Kimarekani 500 ili kuweza kusaidia walemavu mbalimbali katika kulejesha hali zao za kawaida hapa nchini” alisema Bw. Al-Najem.

Aidha katika uzinduzi huo wa Benki ya damu Balozi Al-Najem alijitolea damu unit moja ili kuweza kuchangia benki hiyo ya taasisi ya Mifupa MOI ili kuweza kuhamasisjha na wananchi wengine waweze kuchangia damu kwa msaada wa wagonjwa wengine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Lwezimula alisema kuwa katika kuhakikisha Matibabu ya kibingwa yanapiga hatua nchini waliamu kuanzisha kambi za matibabu kuanzia mwaka 2000 na kufanya taasisi zingine za afya kuiga mfano huo.

“Tunataka kuhamasisha matibabu ya kibingwa kufanyika nchini pamoja na uchangiaji damu kwani damu hiyo haitatumika MOI peke yake bali hata kwenye Taasisi zingne na vituo vya Afya nchini kote” alisema Dkt. Lwezimula.

Sambamba na tukio hilo Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa Wanawake (WOW) Afrika Mashariki walijitolea kuchangia damu ili kuweza kusapoti benki hiyo kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya damu.

“Tumehamasika kuja kuchangia damu ili kuweza kutoa mfano kwa wanachi wengie waweze kujitolea katika uchangiaji huu wa damu ili kujenga taifa lenye watu wenye afya bora” alisema Mkurugenzi wa WOW Bw. Martin Gabone.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad