ACT-Wazalendo Kufanya Maandamano Desemba 8

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

ACT-Wazalendo Kufanya Maandamano  Desemba 8
Idara ya vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo imesisitiza kuwa itafanya maandamano yake ya amani yenye lengo la kupinga vitendo vya utumwa wanavyofanyiwa vijana wa Afrika nchini Libya.

Pamoja na kutojibiwa barua yao ambayo wameliandikia jeshi la Polisi kwenye mkoa wa kipolisi Kinondoni kwaajili ya kuomba kibali cha maandamano hayo lakini wamesisitiza kuwa watafanya hivyo
“Polisi Kinondoni wanasema barua yetu ya maandamano ya tarehe 8/12/17 imetumwa KANDA na mpaka sasa majibu hawajaletewa, wanasema tuulizie tena kesho tunapenda kuujulisha umma kuwa ratiba ya maandamano yetu haijabadilika”, imesema Taarifa ya hiyo kutoka idara ya vijana ACT-Wazalendo.

Idara hiyo ya vijana imepanga kuandamana siku ya Ijumaa Disemba 8 kuanzia saa 4 asubuhi ambapo wataanzia eneo la Leaders Club jijini Dar es salaam na kuishia ofisi za Ubalazi wa Libya nchini zilizopo Upanga jijini Dar es salaam na watatumia barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Hivi karibuni nchini Libya kumeibuka vikundi vya watu ambavyo vinafanya biashara ya utumwa kwa baadhi ya wageni wanaoingia nchini humo hususani wale wahamiaji ambao hufika nchini humo kwa lengo la kuvuka na kuelekea barani Ulaya.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HATUTAKI MAANDAMANO. KAMA KWELI MNAUCHUNGU, FUNGENI SAFARI MUENDE HUKO HUKO LIBYA, MNATAFUTA SABABU YA KUFANYA VURUGU KWA KISINGIZIO CHA LIBYA......TUMEWASTUKIA

    ReplyDelete

Top Post Ad