Askari 14 wa JWTZ Wauawa Katika Shambulio Nchini DR Congo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kuuawa kwa askari 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopo katika operesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Pamoja na askari hao kuuawa, askari wengine 44 wamejeruhiwa na 2 hawajulikani walipo.

Kufuatia vifo hivyo Mhe. Dkt. Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo, Maafisa na Askari wa wote JWTZ, familia za marehemu na Watanzania wote kwa kuwapoteza mashujaa waliokuwa wakitekeleza wajibu wao.

“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na vifo vya vijana wetu, askari shupavu na mashujaa waliopoteza maisha wakiwa katika majukumu ya kulinda amani kwa majirani zetu DRC” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuwa watulivu na kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua zinazostahili baada ya kutokea tukio hilo, na pia amewaombea majeruhi wote wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kawaida.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino, Dodoma

08 Desemba, 2017
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nimesikitishwa sana na kifo Cha Wanajeshi hawa. Lakini najiuliza Je UN hapo kongo inalinda maslahi ya nani?kama si ya nchi kubwa za kimataifa ambazo zinafaidika kutokana na raslimali kuu za uchumi za Congo. Waafrika anzani kuwa wakweli. Anzeni kujiuliza na kupigania haki zenu badala ya hivi vyombo vya kimataifa zinavyowanipulate Waafrica. Kila taifa kuu linaumiliki mkuu wa madini Congo. Madini ya kutengenezea nguvu za nuklia ambazo pia zinatutesa Waafrika wenyewe na dunia nzima.Ni nani asiyejua. Kuanzia Dhahabu, Almasi, na madini ya kutengenezea electonicks zote dubiani. Wapinzani wa Congo wanalijua hili. Raisi wa Congo ni kibaraka cha hawa wazungu wote. Ni aibu kubwa kutumika kwa kutetea maslahi ya Wazungu kupitia UN. MMewapoteza mashujaa, ambao familia zao kamwe hazitakuwa sawa tena kwa kitu si cha ukombozi wa watu wa Congo. Lini Africa itaamka na kuukana utumwa huu.

    ReplyDelete

Top Post Ad