Askofu Aliyetaka Katiba Mpya Ipewe Kipaumbele Ahojiwa na Uhamiaji Kuhusu Uraia Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Askofu Aliyetaka Katiba Mpya Ipewe Kipaumbele Ahojiwa na Uhamiaji Kuhusu Uraia Wake
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Rulenge, Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61), amehojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na uraia wake. Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Askofu Niwemugizi alisema mara ya kwanza alihojiwa Novemba 28 mwaka huu na mara ya pili alihojiwa Desemba 4, mwaka huu.
“Mara ya kwanza niliitwa na kufika ofisi za uhamiaji Ngara, Novemba 28 na mara ya pili niliitwa Desemba 4.
“Niliombwa kibali kinachoniruhusu kuwa nchini, nikashangaa, nikasema mimi ni Mtanzania, nikaambiwa nilete document (nyaraka).
“Nilipeleka hati ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura na cheti cha kuzaliwa, wakasema wataniita tena.
“Baada ya kuitwa mara ya pili, nilipewa fomu ya kujaza ambayo bado naendelea kuijaza hadi sasa.
“Waliniita tena wakasema bado wanataka kujiridhisha ndio maana wanataka nijaze fomu, ninaendelea kuifanyia kazi mpaka nitakapokuwa nimeikamilisha yote,” alisema Askofu Niwemugizi ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC).
Mahojiano kati yake na Mwandishi wa Mtanzania yalikuwa hivi.
Swali: Je, ulizaliwa wapi?
Jibu: Nilizaliwa katika Kitongoji cha Kayanza, Kijiji cha Kabukome, Kata ya Nyarubungo, Wilaya ya Biharamulo.
Swali: Ulizaliwa tarehe ngapi?
Jibu: Nilizaliwa Juni 3, mwaka 1956.
Swali: Ulibatizwa wapi?
Jibu: Nilibatizwa katika Parokia ya Katoke, Biharamulo.
Swali: Elimu ya Msingi na Sekondari ulisoma wapi?
Jibu: Nilisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo na Shule ya Sekondari Nyakato Bukoba (O-level).
Baada ya kumaliza ‘O-level’ niliingia Seminari Kuu ya Ntungamo Bukoba halafu nikatoka hapo nikaenda Kipalapala Tabora.
Swali: Wazazi wako walizaliwa wapi?
Jibu: Walizaliwa sehemu mbalimbali, mama alizaliwa Lusahunga na baba alizaliwa katika Tarafa ya Nyarubungo, Kijiji cha Kabukome Kitongoji cha Kayanza.
Swali: Katika maisha yako yote je, ulishawahi kuhisiwa kuhusu uraia wako?
Jibu: Sijawahi kuulizwa, muda wote nimetumia passport (hati ya kusafiria) ya Tanzania na hakuna aliyewahi kuniuliza suala la uraia.
Swali: Je, unafikiri kwanini hili linajitokeza sasa?
Jibu: Baada ya hivi karibuni kutoa ushauri, kwamba ni vizuri mchakato wa Katiba ukarejewa, watu wali-react, sasa naweza kupata picha nini kimesababisha nianze kuhojiwa.
Swali: Je, Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC) wana taarifa kwamba umeitwa uhamiaji?
Jibu: Sijawataarifu kwa sababu suala hili lilionekana bado liko chini chini, lakini nafikiri nitatafuta namna ya kuwafahamisha juu ya jambo hili.
Swali: Je, mbali na kuwa Askofu, uliwahi kushika nafasi gani katika Kanisa Katoliki?
Jibu: Niliwahi kuwa Rais wa TEC, kuanzia mwaka 2000 hadi 2006 na baadaye nikawa Mkamu wa Rais kuanzia mwaka 2012 hadi 2015.
Swali: Je, una hofu yoyote juu ya usalama wako?
Jibu: Mimi sina hofu na usalama kwa sababu ninajua kufa ni mara moja. Kwa hiyo, ninabaki kivulini, ninazungumza tu ninavyowajibika kama askofu.
UHAMIAJI
MTANZANIA lilizungumza na Msemaji Mkuu Idara ya Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda, ambaye alikiri askofu huyo kuhojiwa.
“Ni kweli anahojiwa na ofisi yetu ya Wilaya ya Ngara, ni suala tu la tuhuma si kwamba ni kweli au la, hivyo itakapothibitika basi itajulikana,” alisema Mtanda.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii ndo tanzania nchi yenye udongo wenye dhambi

    ReplyDelete
  2. Kinacho fanywa na Uhamiaji ni Sawa na Stahiki.
    Ngara na Rusumo ni Karibu sana na ni mikoa ya mpakani ambayo kiurahisi wahamiaji haramu na wavamizi wa Makazi wanaingia kila kukicha. Hassa katika Hiyo miaka unayotajwa

    Askofu ni Lazima aangaliwe mlolongo wa wazazi wake wote..!! Mpaka Turidhike kuwa Huyu ni Wa Kwetu.
    Na kuangalia Familia kubwa yao na Ukoo uko wapi zaidi. Na ikijiri ni wa Kule Basi hatua stahiki Zitachukuliwa... Tanzania ni Ya WATANZANIA NA NI SALAMA.
    Hongera Mama kuiboresha Idara ya Uhamiaji na Kubadilisha mwelekeo mpya. Na Kigoma Kigoma pia ni lazima tufatilie kwa Awamu.

    ReplyDelete

Top Post Ad