Bunduki ya Nassari Yachunguzwa na Polisi Mkoani Arusha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bunduki  ya Nassari Yachunguzwa na Polisi Mkoani Arusha
Wakati mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari akilihusisha tukio la kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na masuala ya kisiasa, polisi inashikilia bunduki ya mwanasiasa huyo kwa uchunguzi.

Polisi mkoani Arusha imesema imeanza uchunguzi wa kina wa kuwasaka washukiwa, huku ikichunguza silaha ya Nassari aina ya shotgun, ikisema tukio hilo lina utata kutokana na mazingira lilivyotokea.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Charles Mkumbo aliliambia gazeti hili kuwa wameanza uchunguzi wa kina ili kubaini endapo kulikuwa na tukio au la.

“Tunaifanyia uchunguzi bunduki yake, tunataka kujiridhisha endapo kulikuwa na tukio au la,” alisema Mkumbo.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema msako unaendelea ili kuwabaini washukiwa na kwamba hawajapata maganda ya risasi zinazodaiwa kutumika katika uvamizi huo.

Juzi Nassari aliwaambia waandishi wa habari kuwa nusu saa baada ya kuwasili nyumbani kwake alisikia hali isiyo ya kawaida ndani ya uzio wa nyumba na baadaye kulisikika milio ya risasi. Alisema mbwa wake aliyekuwa akibweka alinyamaza, hali iliyomfanya achukue silaha yake kujihami.

“Nilipiga risasi tano, kisha kukawa kimya nikaenda kuwaamsha vijana wanaonisaidia hapa nyumbani kuwaeleza tukio lililotokea kisha nikaondoka.”

Alisema waliofanya tukio hilo hawakujua kama ana silaha kwa sababu mwaka 2014 wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, bastola yake ilichukuliwa na polisi na hadi leo haijarudishwa, hivyo kuwa na silaha nyingine kulimsaidia kujibu mapigo.

Katika tukio hilo, Nassari alisema aliwajibu watu hao kwa kupiga risasi tano hewani huku wenyewe wakipiga 12 na moja ilimpata mbwa wake ambaye alimzika juzi katika maeneo ya nyumba anayoishi.

Hivi karibuni mbunge huyo aliwasilisha makao makuu ya Takukuru ushahidi wa CD aliodai kuwa unawahusisha madiwani wa Chadema mkoani Arusha kushawishiwa kuhamia chama taw
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya Maelezo Mbona Utata Mtupu.
    Inaleta maswali mengi zaidi kuliko majibu tarajiwa.
    Joshua Hii Filemu inakula Kwako......!!!!

    Hii siyo Tanzania ileeeee..... Hii ni Tanzania Mpya na mwelekeo Mpya... Umejisahau Dogo...

    ReplyDelete

Top Post Ad