Juuko Murshid Aongezewa Mkataba Mpya Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Juuko Murshid Aongezewa Mkataba Mpya Simba
KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, ameuelekeza uongozi wa timu hiyo umpe mkataba mpya wa kumbakisha klabuni hapo, beki wake kitasa, Juuko Murshid, raia wa Uganda, ikiwa ni muda mfupi baada ya wapinzani wao, Yanga, kumtolea macho kwa ajili ya kutaka kumsajili.

Mcameroon huyo ameyasema hayo wakati mkataba wa Juuko na Simba ukiwa umebakisha siku chache kabla ya kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumatatu kuwa, Omog ameuambia uongozi umpatie mkataba mpya Juuko kutokana na kuwepo kwenye hesabu zake za msimu huu, pia anataka kumtumia kwenye michuano ya kimataifa ambayo Simba watashiriki.
“Kocha amependekeza kuwa lazima Juuko asainishwe mkataba mpya baada ya huu wa sasa wa miaka miwili kumalizika mwezi huu, taarifa ambazo tumesikia ni kuwa wapinzani wetu wanamnyemelea kwa ajili ya kumsajili.

“Unajua kuwa kocha amemjumuisha Juuko kwenye mipango yake ya muda mrefu ya kuwepo hapa ikiwemo kumtumia kwenye michuano ya kimataifa ambayo tutashiriki baadaye mwakani, lakini hata hivyo amekuwa mmoja wa walinzi wetu wazuri hivyo kocha amegoma kuuzwa.
“Lakini pia haiwezekani yeye kuruhusiwa kuondoka kwa sasa kwa sababu kuna uwezekano wa kumuacha Method Mwanjale, hivyo siyo rahisi kujikuta tumewaachia watu wawili wakati wamekuwa nguzo muhimu kwetu tangu msimu uliopita,” kilisema chanzo hicho ambacho kina wadhifa wa juu klabuni hapo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad