Mtulia Ameondoka CUF Kwasababu ya Njaa Zake- Mwingila

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtulia Ameondoka CUF Kwasababu ya Njaa Zake- Mwingila
Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Kinondoni George Mwingila amepinga vikali sababu zilizotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia na kusema hazina ukweli wowote bali akubali kuwa njaa zake ndizo zilizomkimbiza CCM.

Akizungumza leo na Wanahabari Mwingila amesema kwamba Mtulia kuhama CUF ambayo ipo chini ya mwamvuli wa UKAWA kwa madai anakubali kazi rais anayofanya, ni uongo mtupu kwani angeweza kumuunga mkono rais akiwa ndani ya chama chake na siyo kuhama.
"Kwenye ilani yetu ya uchaguzi tuliyoinadi 2015 hapakuwa na ajenda ya kubomolea watu nyumba zao na wala hatukuwa na ajenda ya kununua wanachama wa upinzani wala viongozi wake. Sasa uakuja unasema kwamba unamuunga rais na Chama chake mkono  kwa nini usiseme wazi tu kwamba ni njaa zako. Kama kweli unamuunga Rais mkono kwa nini usimuunge bila kuhama. Mwingila
Ameongeza kwamba "Mbona hata ndani ya Chadema wapo wanaomuunga rais mkono kwa baadhi ya mambo na hata ndani ya CCM wapo wanaotuunga CHADEMA pamoja na Mh. Lowassa mkono mbona wao hawaahami?  Ukweli ni kwamba umefanya usaliti kwa sababu ya njaa.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kinondoni amesema alichokifanya Mtulia ni Usaliti wa hali ya juu na asubiri mshahara wa dhambi hiyo hapa hapa duniani kabla hajaonja mauti.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa tumekuelewa, Mtulia kimemtoa chadema njaa kaenda CCM kwenye shibe.......vipi kuhusu Nyalandu kutoka CCM kwenda chadema, au KUNYA-ANYE-KUKU-AKINYA-BATA-KAHARISHA !!! hahahahaha piipoozzz PWAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Top Post Ad