Nyalandu Amtumia Rais Magufuli Ujumbe Huu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nyalandu Amtumia Rais Magufuli Ujumbe Huu
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, lazaro Nyalandu, jana Disemba 11, 2017 alituma salamu za pole kwa Rais na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia vifo vya askari 14 wa JWTZ waliouawa nchini DR Congo walikokuwa wakilinda amani.

Nyalandu alitumia ukurasa wake wa Facebook kutuma salamu zake za pole kwa Rais Magufuli na familia za askari hao waliouwawa na wale waliojeruhiwa katika mapigano makali yaliyotokea nchini humo Disemba 7 na 8 kati ya askari wa Tanzania na Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) yaliyopelekea askari hao 14 wa Tanzania kupoteza maisha huku wengine 44 wakiwa wamejeruhiwa na wawili wengine kutojulikana walipo.

“Natoa pole kwa Mhe. Rais Magufuli na wanafamilia wote kufuatia kuuawa kwa maaskari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)” alindika Nyalandu.

Miili ya wanajeshi hao iliwasili jijini Dar es Salaam jana kwa ndege maalum ya Umoja wa Mataifa, ambapo ilipelekwa kwenye Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ambapo Desemba 14 itaagwa.
Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga akihojiwa na moja ya vituo vya redio alisema askari wote waliokuwa hawaonekani wamepatikana na uchunguzi unaendelea kwani inaonyesha mmoja wao kama alikuwa ameshikiliwa mateka.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyalandu upinzani utakushinda! Ukiwa upinzani unatakiwa upinge kila kitu hata kama ni kizuri vipi, na penye matatizo unachekelea hata kama hufaidiki chochote tena na kukosoa juu ...... mmmmh WATAKUTIMUA! tehetehetehe

    ReplyDelete

Top Post Ad