Zitto Kabwe Akiombea Uanachama wa FIFA Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

itto Kabwe Akiombea Uanachama wa FIFA Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA)
Mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe ambaye ni mdau mkubwa wa michezo hususani soka amekiombea aunacham wa FIFA chama cha soka cha Zanzibar ZFA.

Hatua hiyo imekuja baaada ya timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA Senior Challenge 2017 inayoendelea nchini Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook Zitto amefunguka ya moyoni akitaka ZFA iwe mwanachama wa shirikisho la soka la kimataifa FIFA pamoja na lile la Africa CAF angalau kwa miaka mitano na inaweza kupiga hatua ambazo TFF imeshindwa.

“Kama hatutaki Zanzibar kuwa Mwanachama wa FIFA kama ilivyo Scotland. Tuseme kwa miaka 5 ijayo kuanzia mwaka huu ZFA ndio mwanachama FIFA na CAF ili TFF ipate muda wa kujipanga. Ndani ya hiyo miaka 5 nawaambia Zanzibar itakwenda AFCON na hata Kombe la Dunia. #MsemaKweliMpenziWaMungu”, ameandika Zitto Kabwe.

Zitto ametoa mfano kuwa Zanzibar ingepata uanachama kamili wa FIFA kama ilivyo kwa nchi za Scotland pamoja na Wales ambazo pia ni nchi dada za taifa la Uingereza lakini zinatambuliwa na FIFA kama mataifa wanachama huku Uingereza ikitambulika kama England.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mhhhh . Zitto amwandikia sepp Blater

    Majibu umeambiwa lini yatakyja kwako au kea Mwakyembe?

    ReplyDelete
  2. Mwakyembe...Dogo anajalibu bahati yake kwako.

    Alivyo wacha playstation kuchaji akaenda nchini twits ili ajalibu kazi za wizala yako.
    Sijui kava ikiwa au umemtolea nje

    ReplyDelete
  3. " Zitto Kabwe Akiombea Uanachama wa FIFA Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA)"
    haya maombi yamepelekwa nchi gani ?
    haya maombi amepelekewa Nani?
    haya maombi yanatarajiwa kujibiwa na baraza lipi?
    haya maombi ni genuine au Feki?

    Huyo Dogo kwa hivi sasa Anarepresent Wizara Gani katika haya Maombi na Waziri wake ni Nani?

    ReplyDelete

Top Post Ad