Aliyemuua Ndugu wa Rihanna Akamatwa na Kufikishwa Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyemuua Ndugu wa Rihanna Akamatwa na Kufikishwa Mahakamani
January 5, 2918 Mwanaume mmoja amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya Tavon Kaiseen Alleyne, 21 ambaye ni ndugu wa mwanamuziki wa kimataifa Rihanna.

Taarifa zilizotolewa na Nation News zimesema, “kijana huyo anafahamika kama Shawayne Dashawn Williams ana umri wa miaka 23, amefunguliwa mashtaka ya mauaji hayo ya Alleyne ambayo yametokea wiki iliyopita katika sikukuu ya Christmas.”

Shawayne amefikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kesi hiyo imeahirishwa na mtuhumiwa amerudishwa gerezani huku hukumu ya kesi hiyo ikipangwa kutolewa January 31, 2018.



Kabla ya tukio marehemu Alleyne alikuwa akitembea karibu na nyumba yake majira ya saa 1 usiku kabla ya kufatwa na mtu asiyefahamika na kisha kupigwa risasi. Hata hivyo Alleyne alikimbizwa hospitali ya Queen Elizabeth iliyopo Bridgetown lakini alifariki dunia.

Wakati huo huo marehemu Tavon Alleyne alikuwa na Rihanna saa moja kabla ya kufariki dunia wakisherehekea pamoja sikukuu ya Christmas.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad