Bodi Ya Mikopo Yawakalia Kooni Waajiliwa Yasema Ukitaka Usilipe Labda Ufe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bodi Ya Mikopo Yawakalia Kooni Waajiliwa Yasema Ukitaka Usilipe Labda Ufe
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) imesema kuanzia Jumatatu ijayo, Januari 8, 2017 itaanza kukagua taarifa za mishahara za waajiri (payroll) ili kubaini waajiri ambao wanawasilisha kiwango kidogo cha mikopo ya wafanyakazi wao ambao ni wanufaika pamoja na waajiri ambao hawawasilishi kabisa pesa hizo kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ili wachukuliwe hatua stahiki.



Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema wanufaika wengi wa mikopo, wakiwemo wadaiwa sugu, wameonesha ushirikiano mkubwa katika kurejesha mikopo yao, hivyo kurahisisha kazi ya kukusanya madeni ya mikopo hiyo.



“Kiasi cha pesa za wadaiwa sugu kilichoiva na kinachotakiwa kuwasilishwa ni Tsh. bilioni 285, hii inajumuisha kuaznia kazi hii ya kukopesha ilipoanza.



“Tangu mwaka jana mpaka sasa tumewapata wadaiwa sugu 26,000, tunashukuru wanufaika hawa wamejitokeza na wanawasilisha mikopo yao. Kuna baadhi ya waajiri wanawasilisha vizuri marejesho ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, wengine hawasilishi na wengine wanawasilisha kiasi kidogo tofauti na asilimia 15 kama sheria inavyotamka.



“Kuanzia Jumatatu, Jan. 8, 2017 tutaanza kukagua taarifa kwenye payroll za waajiri wote waliosajiriwa kubaini waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo wanaodaiwa ili waweze kukatwa. Lengo la kufanya ukaguzi kwenye payroll za waajiri ni kubaini iwapo wana waajiriwa wanadaiwa na HESLB, waajiri wanaowasilisha kiwango kinachotakiwa, wanaowasilisha chini ya asilimia 15 na wanaokata pesa na hawaziwasilishi HESLB,” alisema Badru.



Hata hivyo, Badru amesema wamelazimika kufungua ofisi zao nchi nzima kwa ajili kusimamia malipo ya fedha hizo za mikopo, hasa wale waliotajwa kwenye orodha ya wadaiwa sugu ambapo wamewasambaza wakaguzi nchi nzima, kwa ajili ya kufuatilia waajiri wasiotekeleza wajibu wao wa kuwakata asilimia 15 wanufaika hao waliowaajiri.



Badru pia amewasisitiza watu wote waliowahi kukopa, kulipa wenyewe kwa hiyari kwani bila hivyo, watajikuta wakiingia matatizoni na njia pekee inayoweza kumuokoa mtu aliyekopa asilipe, nio kifo.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad