Chenge Awachukiza Upinzani...... Wasusia Kusoma Maoni Yao Bungeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chenge Awachukiza Upinzani......  Wasusia Kusoma Maoni Yao Bungeni
Msemaji wa upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ally Salehe amesusa kusoma maoni ya upinzani ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kukataa kusomwa kwa baadhi ya maneno yaliyomo katika maoni hayo.

Salehe alikuwa akisoma maoni hayo leo Januari 30 mwaka 2018 kwa niaba ya msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu aliyeko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi Novemba 7 mwaka jana.

Maneno yaliyozuiwa na Chenge kusomwa na upinzani ni kuhusu matukio ya uhalifu nchini, likiwemo la kushambuliwa kwa Lissu.

Salehe alianza kusoma maneno hayo lakini alipofika aya ya nne alikatizwa na Chenge akimtaka asubiri, baadaye kumueleza kuwa lugha iliyotumika katika ukurasa kwa kwanza na pili wa hotuba hiyo si ya kibunge.

Baada ya kauli hiyo, Salehe amesema upinzani unaiamini na unaisimamia hotuba hiyo kwa kuwa wabunge wote wanayo nakala yake, akaomba kuiwasilisha na kurejea kuketi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huhuu hihi mafisadi watakamatwa lini ile mahakama yao sijasikia wakifikishwa ..

    ReplyDelete

Top Post Ad