''Hakuna kama Ronaldinho labda Messi''

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

'Hakuna kama Ronaldinho labda Messi''
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ametoa heshima ya kumuaga nyota wa zamani wa Barcelona na Brazil Ronaldino Gaucho ambaye amestaafu soka kwa kusema hakuna kama yeye labda Messi.


Guardiola ambaye alimuuza Ronaldinho kutoka Barcelona kwenda AC Milan mwaka 2008, amesema wakati Ronaldinho anacheza Barcelona alikuwa mchezaji bora kuwahi kutokea hadi Lionel Messi alipochukua nafasi yake.

"Alikuwa mchezaji mwenye kipaji cha ajabu nafikiri hadi Messi alipokuja kuiteka dunia lakini kiukweli sikuwahi kuona kiwango cha namna ile katika siku za nyuma, hivyo namtakia mapumziko mema na kila la kheri katika majukumu mengine atakayoyaanza'', Guardiola amewaambia wanahabari.

Guardiola pia ameongeza kuwa mafanikio aliyoyapata akiwa Barcelona ilikuwa ni mwendelezo wa kile walichokianzisha Ronaldinho na Rais wa kipindi hicho wa Barcelona Joan Laporta kutokana na ukweli kwamba kabla ya Ronaldinho timu haikuwa kwenye kiwango kizuri.

Guardiola ambaye timu yake ya Manchester City leo itakuwa nyumbani kucheza na Newcastle United amemaliza kwa kusema kuwa anamshukuru Ronaldinho aliondoka vizuri na hana tatizo naye.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad