Hali ya Kingunge Yaimarika Aendelea na Matibabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hali ya Kingunge Yaimarika Aendelea na Matibabu
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema hali ya mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, inaendelea kuimarika baada ya kuanza kupata matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa hospitalini hapo, Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Ngomuo amesema kwa sasa afya yake imeimarika.

"Anaendelea vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema Ngomuo.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete jana Alhamisi jioni alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mwanasiasa huyo.

Kingunge aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, alifiwa na mke wake Pares Mwiru jana Alhamisi saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa.

Neema amesema mke wa mwanasiasa huyo alifikishwa Muhimbili tangu Oktoba 3, mwaka jana.

Wakati Peras akifariki,  mumewe Kingunge anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Awali mtoto wa Kingunge, Kinje Mwiru alisema kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole Mzee Kingunge kwa kuondokewa na fanya Halaka ukishapona uludi CCm
    Hao wanakutumia Tu na sasa Hawana faida na wewe na jukwaa la kuwafagilia hauliwezi tena.

    ReplyDelete

Top Post Ad