Jeshi la Polisi Lafunguka Kuhusu Agizo la Kigwangala

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Lafunguka Kuhusu Agizo la Kigwangala
Jeshi la Polisi limesema limepokea agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla la kuwachukulia hatua watu wanne ndani ya siku saba kwa madai wanashiriki katika mtandao wa ujangili, lakini halifanyi kazi kwa shinikizo.
Akizungumza na Mwananchi leo Januari 26, mwaka 2018 msemaji wa Jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa amesema polisi wanafanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za Jeshi hilo.
Jana,  Kigwangalla mbali na kutoa agizo hilo, amesema watu hao wanne pia walipanga njama za kumuua mwanaharakati, Wayne Lotter na kwamba polisi wakishindwa kuwakamata atawashtaki kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwakalukwa amesema jukumu lao ni kukamata wanapopata shitaka la kuwapo kwa kitu kisicho cha kawaida, kuchunguza na kupeleka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kukamilisha taratibu nyingine.
“Kazi yetu ni kukamata, kuchunguza na kupeleka kwa  DPP kwa ajili ya taratibu nyingine, hatufanyi kazi kwa matamko ya bungeni,” amesema na kuongeza,
“Alichokisema mheshimiwa Kigwangalla nimekisoma kwenye vyombo vya habari akihusisha na suala la mwanaharakati aliyeuawa, sisi hatufanyi kazi kwa kufuata vyombo vya habari vimeandika nini au limetolewa tamko gani au kuna shinikizo gani, tunafanya kwa kufuata taratibu zilizopo.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa nidhamu hawana. Wangekuwa na nidhamu wasingeshirikiana na Lugumi kuwaibia Watanzania mabilioni.

    ReplyDelete

Top Post Ad