Lema Amvaa Lowassa Baada ya Kukutana na Rais Magufuli Ikulu "Umeikosea Tanzania Mema Yapi Umeyaona Katika Serikali Hii?"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lema Amvaa Lowassa Baada ya Kukutana na Rais Magufuli Ikulu "Umeikosea Tanzania Mema Yapi Umeyaona Katika Serikali Hii?"
Baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu,Edward Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu (Chadema) kuonana Rais Magufuli leo. Hatimae Mbunge wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless lema ameibuka na kuhji kuwa ni mema yapi ameyaona katika serikali ya sasa.

Mh. Lowassa alipotoka Ikulu baada ya mazungumzo alisema kuwa “Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo, Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira,lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day,” amesema Lowassa.

Hata hivyo Lema amemhoji Mh. Lowassa kuwa ni mema gani ameyaona katika serikali hii, huku akitolea mfano Mbunge wa Singida Mashariki kuwa anauguza majeraha ya risasi.

“Mh Lowassa,umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu,mema yapi umeyaona katika Serikali hii?Wkt Mbunge Lissu bado anauguza majeraha ya risasi,maiti zinaokotwa,Uchumi unaanguka,Benki zinafungwa ,demokrasia imekufa Bungeni /Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza,” ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad