Maskini..Elias Maguri Amekwama Usajili South Africa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Elias Maguri bado yupo nchini licha ya awali kuripotiwa kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki ligi kuu South Africa.

Prisca Kishamba kupitia Sports Xtra ya Clouds FM amepiga story na Maguri ambaye ameelezea kinachomfanya aendelee kuonekana kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam na sababu iliyopelekea ashindwe kujiunga na klabu ya Polokwane.

“Watu wengi wanategemea kwamba mimi nipo South Africa, lakini kuna sababu ambazo zimenifanya niendelee kuwepo hapa mjini. Awali ilikuwa nimehitajika Polokwane City na nilishasaini mkataba wa awali ambao tulikuwa tumekubaliana wakati nikiwa naenda kwenye mashindano ya Challenge Cup nchini Kenya.”

“Badae niliondoka kwa ajilki ya kwenda kumalizana na watu wa Polokwane nikaiacha timu (Taifa Stars) ikiwa bado kwenye mashindano, lakini kilichotokea kule (South Africa) ndio kinanifanya niendelee kuwa hapa mjini, nilipofika kule makubaliano tuliyokubaliana awali nikaambiwa inabidi kiwango cha fedha kishuke kitu ambacho mimi na wakala aliyenipeleka hatukukubaliana.”

“Kwa sababu klabu na mchezaji wakifikia hatua ya kusaini mkataba wa awali maana yake wameshakubaliana kila kitu lakini mabadiliko ya makubaliano yaliyokuwa yanatakiwa yafanyike baada ya kufika kule ndiyo kitu ambacho hatukukubaliana nacho kwa sababu ukiangalia pia nilikuwa natakiwa nilipe kodi tofauti na ilivyokuwa kule Uarabuni ambako hakukuwa na masuala ya kodi. Unaweza ukajikuta unarudi hapa hauna kitu kwa sababu kiasi kikubwa cha fedha kimetumika kwenye kulipa kodi.”

Maguri amesema kuna ofa kadhaa zipo licha kwamba dirisha la usajili limefungwa kwa hapa nyumbani lakini pia hatokaa tu nyumbani kusubiri hadi dirisha la usajili litakapofunguliwa.

“Ofa zipo licha kwamba tayari dirisha la usajili limeshafungwa kwa hapa nyumbani lakini kuna ofa nyingi ambazo zipo, kwa kuwa mimi ni mchezaji sitoweza kukaa tu nje kwa muda wote huo mpaka dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa, bado kuna michakato inaendelea hadi sasa na mambo yatakapokuwa yamekamilika nitaweka wazi wapi naelekea.”

“Sasa hivi ndiyo watu wanaweza kuwa wanapata habari kwamba nipo nyumbani kwa sababu wengi wanajua nipo south Africa kutokana na taarifa zilizokuwepo hapo mwanzo, kabla ya hapo kulikuwa na vilabu vingi vya hapa nyumbani ambavyo vilitaka nikafanye kazi kwao lakini baada ya kutoka taarifa kwamba naenda nje hata ule mtafutano ukaisha.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad