Mzee Yusuph Ataka Wenye Nyimbo Zake za Taarabu Wazifute

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mzee Yusuph Ataka Wenye Nyimbo Zake za Taarabu Wazifute
Aliyekuwa mwimbaji na Mkurugenzi wa bendi ya Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf amefunguka na kutilia mkazo na kuwaomba watu hususani wanawake ambao bado wana nyimbo zake za Taarab kwenye simu wazifute ili iwe kheri zaidi kwenye imani yake na dini yake


Mzee Yusuf alisema hayo alipokwenda Babati mkoani Manyara katika harakati ya kuzidi kukutana na watu na kuwaomba wazifute nyimbo zake hizo za Taarab kwa kuwa anaamini zinakwenda kinyume na imani yake.

"Niko Babati kuzidi kuwaomba Waislam wanifanyie 'Ihsaan' ya kuzidi kuniombea dua na kuzifuta nyimbo zangu kwenye simu zao kwa ajili ya dini ya 'Allah' iwe kheri na salama. Wengine nyinyi mpaka sasa simu zenu bado zinabalaa naombeni mzifute kwa ajili ya 'Allah' naona haya simu zikipigwa zikaita hizo nyimbo kwani najisikia vibaya sijui nifanyaje" alisema Mzee Yusuf

Aidha Mzee Yusuf alisema kuwa kwa sasa anaogopa na kuwataka wale ambao wanasema wamemkumbuka kwenye masuala ya uimbaji wa nyimbo za Taarabu waache kumkumbuka kwenye mambo hayo bali wamsaidie kwa kuzifuta nyimbo hizo. Mbali na hilo Mzee amewaomba watu wa vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii kufuta kazi zake zote hizo kwa ajili ya hisani ya 'Allah'
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama vipi na yeye arudishe pesa za watu walionunua nyimbo zake huyu mzee ni mjinga na mnafiki mkubwa

    ReplyDelete

Top Post Ad