Wanne Wafariki Dunia kwa Kuofiwa Kula Chakula cha Sumu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wfariki Dunia kwa Kuofiwa Kula Chakula cha Sumu
Watu wanane wamefariki dunia katika mazingira tofauti kuanzia Jumatatu hadi juzi wilayani Kiteto mkoani Manyara, huku chanzo cha vifo hivyo kikiwa bado hakijajulikana.

Wakati wakazi hao wakiripotiwa kufariki dunia, zaidi ya ng’ombe 6,000 wilayani humo wamekufa.

Akizungumza juzi, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa alisema mpaka sasa hawajajua chanzo cha vifo hivyo.

Alisema wataalamu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) wanaendelea na uchunguzi.

Magessa alisema wataalamu hao kwa kushirikiana na wengine wa Wizara ya Afya wameshachukua sampuli kutoka kwa watu waliokufa, ng’ombe na uyoga kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

“Uchunguzi wa awali haujabaini chanzo cha vifo vya watu hawa na mifugo. Bado tunaendelea ili kujua sababu kwa kuwa vifo hivi vimetokea siku tofauti wiki hii,” alisema. Mkuu huyo wa wilaya alisema, “Watu wamekuwa wakizungumza mambo mengi kuhusu chanzo cha vifo, ikiwamo kula nyama ya ng’ombe na wengine wakidai kuwa walikula uyoga.”

Alisema baadhi ya wafugaji wilayani humo wanadai chanzo cha ng’ombe kufa ni kula majani baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko. “Majina ya waliofariki dunia bado hatujayapata ila wawili walifariki katika Kata ya Kiperesa, wanne katika Kijiji cha Emat, Kata ya Magungu na wengine wawili bado hatujajua walikuwa wakazi wa kijiji kipi.”

Alisema, “Baada ya ukame, mvua kubwa ilinyesha na majani mapya kuota, sasa wanasema ng’ombe walipokula nyasi hizo ndipo wakafa ila bado tunafanya uchunguzi.”

Alisema mizoga ya ng’ombe hao imekutwa maeneo tofauti, mingine ikiwa barabarani na porini. Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi wa eneo hilo kuwa watulivu akisema Serikali inafanya uchunguzi kubaini sababu ya vifo vya watu hao na mifugo.

Mkazi wa Kata ya Kiperesa, Shabani Khamis alisema vifo hivyo vimewashangaza kwa kuwa chanzo chake hakijafahamika.

“Hata hatujui tatizo ni nini, pengine tuiachie Serikali kufanya uchunguzi na kubaini chanzo. Hayo mambo ya uyoga au kula mboga zenye sumu si ya kuyasema kwa sasa,” alisema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad