Ajibu Kuongeza Nguvu Leo Mechi Dhidi ya Shelisheli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ajibu Kuongeza Nguvu Leo Mechi Dhidi ya Shelisheli
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ibrahim Ajibu na chipukizi anayekua kwa kasi, Yohana Nkomola wamerejesha matumaini kwenye timu hiyo na leo Jumamosi huenda wakawepo kwenye orodha ya kikosi kitakachoivaa St Louis ya Shelisheli. Yanga itawakaribisha wapinzani wao hao katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ajibu anarejea uwanjani akitokea kupona majeraha ya goti aliyoyapata kwenye Ligi Kuu Bara wakati timu hiyo ilipovaana na Azam FC na Nkomola yeye alipata maumivu ya misuli katika mchezo wa Ruvu Shooting.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu, alisema wachezaji hao wameanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzao juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Bavu alisema kurejea kwa wachezaji hao kumeimarisha kikosi chao kutokana na kupunguza idadi ya wachezaji majeruhi waliokuwa wanaiandama timu hiyo.

“Niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga kuwa, wachezaji wetu muhimu waliokuwa majeruhi Ajibu na Nkomola wamepona na jana (juzi Jumatano) walianza mazoezi ya pamoja na wenzao.

“Kwa maana hiyo hivi sasa wapo fiti kucheza mechi ya kimataifa kama kocha akihitaji kuwatumia, lakini mimi kama kocha niseme wapo fiti kwa ajili ya kuipambania timu yao ya Yanga. “Kipa wetu Rostand (Youthe) aliyepata majeraha ya enka kwenye mechi iliyopita na Lipuli FC naye anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti kabla ya kuanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzake,” alisema Bavu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad