Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa Bei Juu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa Bei Juu
kawaida kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kukuletea bei mpya za Mafuta nchini kila Jumatano ya kwanza ya mwezi na leo February 7, 2018 imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikiongezeka.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ambapo amesema bei za rejareja zimeongezeka kwa Petroli ikiwa ni Tsh59 sawa na asilimia 2.70, Dizeli Tsh46 (sawa na asilimia 2.30), na mafuta ya taa kwa Tsh24 (sawa na asilimia 1.17).

Amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambazo kwa Petroli ni Tsh58.57 sawa na asilimia 2.85, Dizeli kwa Tsh46.48 (sawa na asilimia 2.44) na mafuta ya taa kwa Tsh23.75 (sawa na asilimia 1.24).

“Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Januari 3. Bei za mafuta ya taa hazijabadilika kwa sababu hakuna yaliyoingizwa nchini kupitia bandari hiyo Januari,” -Mchany.

“Ongezeko la bei za mafuta ya petroli na dizeli katika Mkoa wa Tanga linatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji,” -Mchany.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad