Haya Hapa Mapya ya Lulu Akiwa Gerezani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Haya Hapa Mapya ya Lulu Akiwa Gerezani
IKIWA ni takriban siku 85 tangu staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aswekwe lupango katika Gereza la Segerea, Dar kwa kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, mapya akiwa gerezani yameanikwa.



Mapya hayo yamebainika baada ya gazeti hili kutaka kujua kinachoendelea kwa sasa kwenye maisha ya Lulu ambapo Jumapili iliyopita, saa 6 mchana mwandishi wetu alitinga katika gereza hilo kwa lengo la kumuona na kuzungumza naye lakini alikumbana na vizingiti.



Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa maafisa wa magereza aliyekutwa eneo la getini na kugoma kutaja jina lake akidai si msemaji alisema:

“Kwani wewe ni miongoni mwa wale wana familia wanaokuja kumuona? Hapa wanaoruhusiwa ni wale tu ambao ni wanafamilia vinginevyo labda uje nao.”



Hata hivyo, mwanahabari wetu alijaribu kumlainisha afisa huyo na kumuweka wazi nia yake ya kufika gerezani hapo ambapo ulifika wakati akafunguka mambo mbalimbali mapya kuhusu Lulu.

Alisema mrembo huyo kwa sasa ni shavu dodo, anaendelea vizuri na kifungo chake na tangu aingie gerezani, hajawahi kuugua.

“Yani kwa kweli amenenepa kabisa tofauti na hata alivyokuja. Anaendelea vizuri na hajawahi kuugua ugonjwa wowote tangu afike,” alisema ofisa huyo.



AWASHANGAZA WANAOMTEMBELEA

Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kuwa, mbali na kutoumwa na kunenepa, muda wote mrembo huyo amekuwa mtu wa kutabasamu na kuwatia moyo wanaokwenda kumsalimia, jambo ambalo linawashangaza kwa sababu huwa wanahuzunika huku yeye akijiamini na kuwafariji.



“Anawashangaza kwa kweli ndugu zake ambao wanakuja kila wiki kumuona, yani yeye anakuwa na furaha, anawapa moyo utafikiri yeye ndio yupo sehemu nzuri kuliko ndugu zake,” alisema ofisa huyo na kuongeza:

“Huyu binti kwa kweli sasa hivi anasali sana. Na mara nyingi huwa namsikia akiwaambia ndugu zake kuwa wasihuzunike, wachukulie kama tu yupo shule ya boarding atatoka tu.”


Muna.

MUNA AFUNGUKA

Amani lilimtafuta na kufanikiwa kukutana na rafiki ambaye ni kama ndugu kwa familia ya Lulu, Rose Alphonce ‘Munalove’ ambaye alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo makubwa ya Lulu na kwamba amekuwa akiwafariji wanapokwenda kumtembelea, alikiri kuwa ni kweli.

“Ni kweli anatushangaza hata sisi, kwanza kanenepa na anaonekana mwenye furaha maana wakati mwingine tukienda kumuona tunakuwa na simanzi lakini yeye anakuwa mfariji wetu akisema kwamba ipo siku atatoka na kuwa huru tena,” alisema Muna ambaye inadaiwa kila wiki lazima amtembelee Lulu gerezani.



MSIKIE MAMA LULU

Alipopigiwa simu mama Lulu, Lucresia Kalugira ili kueleza juu ya hali halisi ya mwanaye huyo, alitokwa povu huku akidai kwamba hataki kusikia magazeti.

“Sitaki kusikia habari za magazeti au waandishi wa habari maana mimi siyo supastaa na kuhusu mwanangu naombeni mmuache maana tayari yupo gerezani,” alisema mama Lulu.



TUMEFIKAJE HAPA?

Itakumbukwa kuwa hukumu ya Lulu kutumikia kifungo cha miaka miwili ilitolewa Novemba 13, mwaka jana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Sam Rumanyika baada ya mahakama kujiridhisha kuwa aliua bila kukusudia.



CHANZO CHA KESI YAKE

Lulu alihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua bila kukusudia, muigizaji Kanumba aliyepoteza maisha Aprili 7, 2012, baada ya kutokea ugomvi kati yao majira ya usiku wakiwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Vatican, jijini Dar es Salaam.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad