Kamati ya Nidhamu Yamfungia Mwamuzi Kuchezesha Soka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kamati ya Nidhamu Yamfungia Mwamuzi Kuchezesha Soka
Shirikisho la soka la Ufaransa (FFF) kupitia kamati ya nidhamu inayosimamia ligi kuu nchini humo Ligue 1 imemfungia miezi sita mwamuzi Tony Chapron kwa kosa la kumpiga mchezaji kisha kumwadhibu kwa kadi.

Sehemu ya taarifa ya FFF imeeleza kuwa, ''Baada ya kumsikiliza Tony Chapron na kusoma ripoti ya kamisaa wa mchezo, kamati imeamua kumfungia kwa muda wa miezi sita, pamoja na wiki tatu ambazo alisimamishwa".

Disemba mwaka jana kwenye mchezo wa Ligue 1 kati ya Nantes dhidi ya PSG Chapron alikwatuliwa kwa bahati mbaya na mchezaji wa Nantes Diego Carlos lakini alilipiza kwa kumkwatua mchezaji huyo kisha kumwonesha kadi ya pili ya njano.

Baada ya mechi Tony Chapron alisimamishwa kabla ya usiku wa kuamkia leo kamati ya nidhamu kutangaza kumfungia miezi sita mwamuzi huyo ambaye amechexzesha mechi zaidi ya 400 za Ligue 1 tangu mwaka 2004.

Kabla ya tukio hilo Chapron mwenye miaka 45 alikuwa ametangaza kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho kama mwamuzi na alitarajia kustaafu mwishoni mwa msimu wa 2017/18.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad