Makonda Apata Tena Msaada wa Majengo Matano ya Walimu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda Apata Tena Msaada wa Majengo Matano ya Walimu
Ubalozi wa China nchini Tanzania umemzawadia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda majengo matano ya kisasa kwaajili ya ofisi za walimu baada ya kupeleka ombi la kuhitaji msaada wa kuboresha mazingira ya walimu.


Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke amesema kwa miezi mitatu aliyoishi hapa nchini tangu alipoteuliwa kuwa balozi ameshuhudia maendeleo makubwa na serikali ya mkoa hivyo wameona wasikae kimya kwenye jambo linalolenga kuleta ukombozi wa uchumi kupitia elimu.

Majengo hayo ambayo  yatajengwa kwenye wilaya tano za mkoa wa Dar es salaam ambapo leo Mh. Makonda ameweka jiwe la msingi pamoja na kukabidhi Ramani ya jengo kuashiria kuanza kwa ujenzi huo kwenye shule ya sekondari Makumbusho.



Akiushukuru Ubalozi huo, Makonda amesemaujenzi wa majengo hayo kwa kiasi kikubwa unaenda kupunguza mateso ya walimu kufanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kufanya kazi kwenye madarasa.

Amesema dhamira yake ni kuboresha mazingira ya walimu ni kuwawezesha kutoa elimu bora itakayowezesha Taifa kuwa na wataalamu wa kutosha.

Majengo hayo yanatarajiwa kuwa na na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi, Ofisi ya walimu wote, ukumbi wa mikutano, chumba cha kuhifadhi mitihani, vifaa vya michezo, chumba cha muhasibu, chumba cha kubadili nguo, mapokezi, vyoo, bafu ikiwa na samani za kutosha.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad