Maneno ya Izzo B, Rama Dee na Niki wa Pili Muda Mchache Baada ya Sugu Kuhukumiwa Miezi 5

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Izzo B, Rama Dee na Niki wa Pili Waguswa na Kifungo cha Sugu Waandika Ujumbe Huu
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na mwenzake Emmanuel Masonga wamehukumiwa kwenda jela miezi mitano na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya leo Februari 26, 2018 baada ya kukutwa na hatia kutumia lugha ya fedhea dhidi ya Rais Magufuli.


Baada ya kuhukumiwa kwenda jela baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva wamefunguka yao ya moyoni kuhusu tukio hilo huku wengine wakimtia moyo kuwa gerezani siyo kaburini hivyo atamaliza muda wake na kurudi uraiani kuwapigania wananchi wa Mbeya.

"Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini 'stay strong' Jongwe" aliandika Niki wa Pili

Kwa upande wake msanii Rama Dee yeye amesema kuwa ameumizwa sana na bahari ya Sugu kufungwa jela miezi mitano na kudai si picha nzuri katika nchi yetu kwa mambo kama haya.

"Nasikitika sana kwa hii habari kama msanii pia kama rafiki wa Sugu, hii si picha nzuri" Rama Dee

Aidha msanii Izzo Bizness ambaye anaiwakilisha Mbeya vizuri katika muziki wa Hip hop pia ameonyesha hisia zake na kumtaka Mbunge huyo kuwa mvumilivu na kusimama imara katika kipindi hiki.

Mbali na huyo Rapa Roma Mkatoliki alikuwa na haya ya kusema juu ya kifungo cha Sugu "Hata hili lipatita' stay strong Joseph Zaburi 35: 1-28 "
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa ilikuwa wasanii wote kwa pamoja kulaani . huu ni uonevu. Nanua wasanii wengi wapo ccm, ni tatizo kufikiri kichama badala ya kitaifa. Sugu amefungwa kisiasa tu. Wengi wasanii ni waoga, au hamjauelewa mfumo wa vyama vingi, au hamko huru.inasikitisha kwani hakustahili kufungwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. acheni kutukana wakubwa, nani alimwambia atukane

      Delete
  2. Inasikitisha Mahakama haikuwatendea haki Watanzania kwa kutoa adhabu stahiki kwa Sugu kana kwamba kuna upendeleo fulani labda kwakua yeye ni mbunge kwani kifungo cha miezi mitano jela ni kidogo kama utafualia uchafu na uozo wa tabia za Sugu kama kiongozi wa Umma utakubaliana nami yakwamba alistahili adhabu kali zaidi. Unakumbuka wakati Sugu aliponyanyua kidole chake cha kati kuwaonyeshea wabunge wa CCM bungeni? Kitendo kile peke yake kilistahili kumsekwa Sugu mwaka mmoja jela. Sugu hakuwa anaonyesha kidole chake cha kati kwa wabunge wa CCM pekee bali alikuwa akiwatia vidole watanzania wote. Ni moja ya mambo ya fedheha kabisa kwa kiongozi wa Umma kuyafanya hadharani. Sugu ameishi Marekani anaelewa fika uzito wa kumnyooshea mtu kidole cha kati na consequence au madhara unayoweza kusababisha kutokana na counter attack kutoka kwa yule uliemnyooshea kidole cha dharau. Huwezi kuyapeleka mambo ya kipuuzi ya mitaani kwenye sehemu serious kama bunge. Tabia hiyo mbovu ya Sugu kama kiongozi wa Umma ilitia shaka labda inasukumwa na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya. Binafsi kama ningekuwa na uwezo wa kukata rufaa kutokana na kutoridhika na adhabu aliopewa ningefanya hivyo ili aongozewe adhabu kubwa zaidi. Miaka mitano jela ni mingi kulingana na kosa lake lakini miezi mitano jela ni kama wamempeleka vacation.

    ReplyDelete

Top Post Ad