Yanga Yapewa Muda wa Kuimaliza Botswana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Yapewa Muda wa Kuimaliza BotswanaYANGA kwa sasa watakuwa na uhakika wa kuwamaliza wapinzani wao, Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa hapa nyumbani baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwafutia mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga watakutana na Wabotswana hao katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar, Machi 6, mwaka huu.

Yanga ambao leo Jumatano watacheza na Ndanda FC, walipangwa kucheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro Machi 3, mwaka huu ambapo kwa sasa mchezo huo umesogezwa mbele.

Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa ameliambia Championi Jumatano, kuwa: “Tuliiomba Bodi ya Ligi ya mchezo wetu na Mtibwa Sugar usogezwe mbele na tayari tumepokea barua kutoka kwao ikionyesha kwamba mechi yetu hiyo haitakuwepo kwenye tarehe hiyo. “Muda huu utakuwa sababu tosha kwetu kujiandaa na kufanya vizuri katika mechi hiyo kwa sababu wachezaji watakuwa na muda wa kutosha wa kupumzika,” alisema Mkwasa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad