Eric Omondi Awatolea Uvivu Wanaoendeleza Mjadala wa Video Yake ya Utupu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Eric Omondi Awatolea Uvivu Wanaoendeleza Mjadala wa Video Yake ya Utupu
Mchekeshaji mahiri wa nchini Kenya, Eric Omondi amefunguka na kuwashangaa baadhi ya watu wanaoendelea na mjadala wa video ya utupu iliyosambaa mtandaoni na kuacha vitu vyenye tija ambavyo watu wanapaswa kuvijua imekuwaje.


Omond ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa) kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kushambuliwa kwa maneno makali na mashabiki zake na kutaka apelekwe Mahakamani ili aweze kujibu mashtaka ya udhalilishaji kutokana na kuweka mtandaoni 'video' iliyokuwa ikimuonesha akiwa utupu akiogelea katika mto na watoto.

"Sasa hivi kila kituo cha redio, 'blogger' pamoja na magazeti wanataka stori yangu, macho yao yote yapo kwangu, wanataka 'attention' yangu. Labda ni muda muafaka kwangu mimi kusema kuzungumza, kwasababu kuna mtu anaweza akasoma hichi nilichoandika na ninasali watu sahihi wasome",amesema Omondi

"Vipaumbele vyetu kama taifa vinaweza kuwa havijakaa sawa. Wakati tunajadili kuhusiana na kijana wa kiafrika ambaye aliogelea mtoni, kijana mdogo wa chuo alipigwa risasi na kufariki  na hospitali ya taifa ikamfanyia upasuaji mgonjwa mwingine asiyehusika. Ninatamani kujua stori ya kijana huyo. Alikuwa anasomea nini? ndoto zake ni zipi? alikuwa ni mtoto wa pekee", amesema Omondi.

Pamoja na hayo, Eric Omondi ameendelea kwa kusema "ninataka kuongea na kila mvulana na msichana, kila ndoto inaweza kutimia kuwa kweli. Kama unataka kuruka usikubali mtu mwingine akuambie huwezi au kukatisha tamaa, hata kama ni kuna nguvu ya mvutano ruka. Ila unatakiwa kuwa tayari kupanda milima na kushuka kwenye mabonde lakini mwisho wa siku utafika kileleni".

Kwa upande mwingine, mchekeshaji huyo amewatia moyo vijana wenzake waendelee kupambana na huku wakumbuke kumtanguliza Mungu mbele ili wafike wanapopahitaji.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad