Idriss Achoka Kuwa Single Akwapua Kifaa Kipya Kitakachoziba Pengo la Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Idriss Achoka Kuwa Single Akwapua Kifaa Kipya Kitakachoziba Pengo la Wema Sepetu
MCHEKESHAJI kiwango Bongo na mshindi wa Shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan, anadaiwa kunasa kifaa kipya kutoka nje ya nchi anayetambulika kwa jina moja la Aya, ambaye ‘kitamliplesi’, mwanadada kutoka Bongo Movie, Wema Sepetu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake.



Ijumaa limepenyezewa ubuyu na ‘sosi’ kwamba Idris, ameamua kumnasa Aya ambaye ana jina kubwa nchini Tunisia na kwamba ndiye mrithi wa Wema kwani tangu aachane naye hajapata mrembo mwenye jina kubwa kuliko yeye na aliyempenda kwa dhati.



“Nyie muulizeni tu Idris atawaambia. Sasa anakifaa kipya kutoka nje, kinaitwa Aya na hivi karibuni alitua Bongo wakafanya matanuzi hadi picha zingine zikasambaa wakiwa swimming pool wakiogelea kimahaba,” alisema sosi huyo.



Baada ya kutumegea ubuyu huo, Ijumaa liliweza kumsaka Idris,ambapo baada ya kupatikana alifunguka;


“Aya ni kweli ninamfahamu. Ni mtu wangu wa karibu saana lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi. Tumekutanishwa na programu ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na yeye alikuja Bongo kwa ajili ya kikao cha project hiyo,” alisema Idris.



Hata hivyo, gazeti hili lilizidi kumbana Idris, kwamba kukutana kwa ajili ya project ndiyo waonekana mpaka hotelini, kwenda kuogelea na kwenye mapozi tata kama mtu na mpenziye, ambapo alijibu kukutana huko kulitokana na ukaribu wao tu na si vingine.



“Kama nilivyosema ni mtu wa karibu sana. Sasa kwenda naye kuogelea kwangu sioni kama ni tatizo, ijulikane tu Aya ni mtu wangu wa karibu.” Alimaliza Idris.



Idris aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema ambapo uhusiano wao ulizidi kuwa maarufu ilipokuja kujulikana kwamba Wema amenasa ujauzito ambao ulidumu kwa wiki kadhaa na kutoka kwa bahati mbaya. Hata hivyo, uhusiano wao ulikuja kuvunjika huku sababu za kuachana zikifi chwa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad