Ishu ya Abdul Nondo Yafikia Pagumu IGP, DCI NA AG Waitwa Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ishi ya Abdul Nondo Yafikia Pagumu  IGP, DCI NA AG Kufikishwa Mahakamani Mahakama Kuu nchini  imetoa wito wa kuwaita DCI, IGP na AG kufika mahakamani siku ya Jumatano ya tarehe 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi  (TSNP) Abdul Nondo.


Taarifa za wito huo umetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole ambaye ametoa taarifa hiyo fupi kupitia kwenye ukurasa wake maalum wa Twitter.

Kambole amesema "Wito umetolewa leo Mahakama kuu mbele ya Jaji Samejikwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani 21/03/2018 kujibu kesi ya Abdul Nondo".

Akizungumza na www.eatv.tv Kambole amesema washitakiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa Jumatano, Sirro ameitwa kwasababu yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini hivyo vituo vyote na polisi wapo chini yake lakini bado Nondo amekuwa hapatikani katika vituo vya polisi.

Aidha Kambole amesema kuwa katika jalada lililofunguliwa leo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), naye kahusishwa kwa sababu mara ya mwisho Nondo alipokelewa na yeye alipofikishwa Dar es salaam kutoka Iringa na kwamba alimchukua kama muathirika wa tukio la utekwaji na siyo mshtakiwa.

Hata hivyo Kambole amesema ameshafanya jitihada nyingi za kutaka kuonana na mteja wake lakini hadi sasa juhudi zake hazijafua dafu.

Abdul Nondo anashikiliwa na jeshi la polisi tanguMachi 7, ambapo awali aliripotiwa kupotea kusikojulikana na kesho yake kujikuta Iringa, ambapo Kamanda wa Polisi  Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mpaka sasa wanamshikilia Nondo kwa ajilili ya upelelezi na watakapokamilisha watamfikisha mahakamani.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad