Jacob Zuma Kuburuzwa Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jacob Zuma Kuburuzwa MahakamaniRais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani mwezi Aprili kwa makosa 16 yakiwemo ya kutumia vibaya ofisi wakati akiwa madarakani na ufisadi.

Duru za habari nchini Afrika Kusini kusini likiwemo gazeti la News24 limeeleza kuwa Zuma atafikishwa kizimbani katika Mahakama Kuu mjini Durban tarehe 6 Aprili 2018 kwa makosa 16.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa bodi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo, Brigedia Hangwani Mulaudzi amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii watawasilisha barua kwa mawakili wa Zuma juu ya wito huo.

Mulaudzi amesema kuwa Zuma atakabiliwa na mashtaka makubwa 16 ambapo rushwa na Matumizi mabaya ya ofisi yanatajwa kuwa ni moja ya mashtaka yaliyopewa kipaumbele.

Imeelezwa kuwa Jacob Zuma alifanya malipo ya risiti 783 kiholela, kwenye ununuzi wa silaha na vifaa vya jeshi nchini Afrika Kusini ambapo inakadiriwa kuwa ametumia mabilioni ya fedha kwenye ununuzi huo.

Mwaka 2012, Zuma aliingia kwenye kashfa nzito baada ya kutengeneza nyumba yake ya kifahari kwa kutumia fedha za serikali, ambapo alitumia zaidi ya dola milioni 25 za kimarekani.

Hata hivyo, kashfa hiyo ilitetewa na baadhi ya wabunge wa chama tawala nchini humo ANC, ambapo walieleza kuwa ukarabati huo ulizingatia vigezo.

Mnamo Februari 14, 2018. Mzee Zuma alitangaza kung’atuka madarakani baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wanachama wa ANC na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu wake wa Rais, Cyril Ramaphosa.


Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kisiasa barani Afrika wanasema kuwa hatua ya Zuma kufunguliwa mashtaka ni mpango wa chama cha ANC kujisafisha, ili kujiwekea nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu ujao wa urais mwakani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad