Kisa-100 ya Roma Chadema Wataka Basata Ichukuliwe Hatua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Patrick Ole- Sosopi amesema Baraza la Sanaa la Taifa linapaswa kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kusimamia majukumu ya kazi zao ndiyo maana walishindwa kuzichukulia hatua nyimbo zinazodaiwa kutokuwa na maadili.


Akizungumza na vyombo vya habari, Ole- Sosopi amesema hayo leo ambapo amesema kwamba kama nyimbo zimeweza kusikilizwa kwa muda mrefu basi ni wazi maadili na jamii zilishapotoka kwa muda mrefu kutokana na uzembe wa viongozi waliopaswa kuchukua hatua za haraka pindi  nyimbo hizo zilipoka.

Mwenyekiti huyo anayewakilisha vijana wa CHADEMA Tanzania, ameongeza kuwa hakuna mtu anayependa kusikia au kuona nyimbo zenye maudhui mabaya lakini anashangaza na jinsi baraza hilo linavyofanya kazi kwa mashinikizo huku akiongeza kwmba adhabu zilizotolewa kwa wasanii hazistaili.



Pamoja na hayo Sosopi amemtaka Naibu Waziri, Juliana Shonza kutengua adhabu yake hiyo kwani sheria haimpi yeye mamlaka ya kutoa adhabu alizotoa na badala yake wajibu huo upo chini ya BASATA.

Hapo jana Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo alitangaza kumfungia Msanii Hip Hop bongo, Roma Mkatoliki kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii huyo kudharua wito wa BASATA na Naibu Waziri huyo w kurekebisha wimbo wao wa 'KIBAMIA' waliouimba yeye na Stamina (ROSTAM)
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Afadhali chadema sasa muhamia kwenye muziki, maana siasa imewashinda na maandamano hakuna tehetehe

    ReplyDelete

Top Post Ad