Mwanza Yatajwa Kinara kwa Watumishi wa Ndani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanza Yatajwa Kinara kwa Watumishi wa Ndani

Mikoa ya Kagera na Mwanza imetajwa kuwa vinara kwa wenyeji wake ambao ni watoto wenye umri chini ya miaka 14 kufanya kazi za ndani maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya mikoa hiyo.

Hayo yameelezwa jijini Mwanza leo Machi 15 na mjumbe wa sekretarieti ya kuzuia na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, Ahmad Mwen-dadi wakati wa mafunzo maalumu kwa watekelezaji wa sheria za kupambana na usafirishaji wa watoto kwa ajili ya kazi za majumbani maeneo ya mijini.

Amewaeleza  wajumbe wanaohudhuria mafunzo hayo yanayoratibiwa na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la Kiwohede, kuwa baadhi ya watoto wanaosafirishwa kwenda mijini kufanya kazi za ndani hujikuta wakifanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na waajiri wao au ndugu wa familia wanakofanya kazi.

Mikoa mingine yenye idadi kubwa ya watoto wanaosafirishwa kwenda mijini kufanya kazi  kwa mujibu wa Mwen-dadi ni Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Dar es Salaam. 

Mafunzo hayo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwohede, Justa Mwaituka yanahudhuriwa na askari polisi kutoka dawati la jinsia, watendaji wa idara ya mahakama, ofisi ya Mwanahseria Mkuu wa Serikali, Idara ya Uhamiaji, maofisa ustawi wa jamii na maofisa kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad