Mwigizaji Video za Utupu Adai Alitishiwa Kuhusu Donald Trump

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwigizaji Video za Utupu Adai Alitishiwa Kuhusu Donald Trump
Mwigizaji wa video za utupu Stormy Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, amesema alitishiwa na kutakiwa kukaa kimywa kuhusu kufanya tendo la ndoa na Donald Trump mwaka 2006.

Ameambia kituo cha runinga cha CBS News kwamba mwanamume mmoja alifika kwake alipokuwa kwenye maegesho ya magari mjini Las Vegas mwaka 2011.

Mtu huyo ambaye hakumfahamu anadaiwa kumwambia "mwache Trump", kisha akamtazama binti mdogo wa mwigizaji huyo na kuongeza: "Itakuwa aibu sana iwapo jambo litamtendekea mamake."

Bw Trump amekanusha vikali kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji huyo.

Mawakili wa Bw Trump wanataka kulipwa fidia ya $20m (£14m) na mwanamke huyo, wakisema alikiuka makubaliano ya kuweka siri ambayo aliyatia saini katika ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Ameambia kipindi hicho cha Dakika 60, ambacho kilipeperushwa hewani Jumapili jioni, kwamba mwanamume huyo alimjia baada yake kukubali kusimulia kisa chake kwa jarida moja.

"Nilikuwa kwenye maegesho ya magari, nilikuwa naelekea kwenye kikao cha mazoezi niliwa nimembeba binti wangu mchanga," alisema.

"Mwanamume alinijia na kuniambia, 'Mwache Trump. Sahau taarifa hiyo'. Kisha, aliinama na kumtazama binti wangu na kusema, 'Ni msichana mdogo mrembo sana. Itakuwa ni aibu sana iwapo jambo litamtendekea mamake'. Na hivyo tu, akaondoka."

Rais huyo alikuwa kituo chake cha gofu na hoteli cha Mar-a-Lago jimbo la Florida wikendi lakini alirejea White House kabla ya kipindi hicho kurushwa hewani.

Bi Trump hata hivyo alisalia Florida, msemaji mmoja wa White House alisema.

Nini kinadaiwa kutokea 2006?

Bi Clifford aliambia CBS kwamba mara pekee ambapo alifanya ngono na Bw Trump ni wakati alipomwalika kwa chakula cha jioni kwenye chumba chake cha hoteli.

Anasema Bw Trump alimuonesha jarida lililokuwa na picha yake kwenye jalada.

Anasema alilichukua jarida hilo na kumgonga Trump nalo makalioni kama utani.

"Aligeuka na kuteremsha suruali yake chini kidogo, unajua, alikuwa na suruali ya ndani na vitu vingine, na nilimgonga kidogo kidogo kwa utani," anasema.

Bw Clifford anasema ingawa hakuvutiwa kwa vyovyote vile na Bw Trump, alifanya mapenzi naye wakati huo, akisema: "Sikukataa. Mimi si mwathiriwa."

Bw Trump, anaongeza, alikuwa amedokeza kwamba kulikuwa na uwezekano angeshirikishwa kwenye kipindi chake cha runinga cha The Apprentice.

Anasema alichukulia mkutano wao kuwa sawa na "mkutano wa makubaliano ya kibiashara".

Bi Clifford ameambia CBS alipokeza "fedha za kukaa kimya" kutoka kwa wakili wa kibinafsi wa Trump kwa sababu alikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa familia yake.

Amewahi kusema awali kwamba alilipwa $130,000 na wakili huyo Michael Cohen kusalia kimya kuhusu uhusiano wao huo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2016.

Bw Cohen alithibitisha Februari kwamba alimlipa mwanamke huyo lakini hakusema alimlipa kwa niaba ya nani.

Wakosoaji wa Bw Trump wamedokeza kwamba kuna uwezekano pesa hizo zilikuwa sehemu ya mchango wa pesa haramu za kampeni.

Bw Cohen alisema mwezi jana kwamba Bw Trump na kampuni yake ya Trump Organization hawakuhusika katika kulipwa kwa pesa hizo.


Bi Clifford ni mmoja kati ya wanawake watatu ambao wameanza kesi dhidi ya Rais Trump kuhusu madai ya uhusiano wa kimapenzi au udhalilishaji.

Wakili wake Michael Avenatti ameambia BBC kwamba kesi ya mteja wake ni tofauti na wengine kwa sababu inahusu "visa vya kutolewa vitisho na mbinu ambazo zilitumiwa kumnyamazisha mteja wangu."

"Nafikiri ni kisa cha kustaajabisha na kinafaa kuwashangaza sio tu Wamarekani bali pia watu katika mataifa yaliyostaarabika ya magharibi," amesema.

Ameongeza: "Hivi sivyo watu walio madarakani wanavyofaa kuendesha shughuli zao."
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad